Eymael analalamika kwamba alikuwa analenga kuwaleta wachezaji wa nchi za kigeni katika dirisha hili la uhamisho lakini kamati hiyo ikaamuru asajili wale wa kutoka Afrika Mashariki tuu.
“Sielewi kwanini vinara wa klabu wananizuia kuwaleta wachezaji wa kutoka nje ili hali wengine wanapatikana kwa bei rahisi kuliko hata wa hapa nchini. Baadhi ya niliotambua wana uzoefu mkubwa na wana uwezo,”
Eymael alifoka katika taarifa aliyoitoa hoteli mmoja jijini Nairobi.
“Sitaki kushinikizwa na yeyote na kama hali ya mambo hayatabadilika hapa katika awamu ya pili ya musimu, mimi ndiye nitakaye laumiwa kwa sababu nilikuja hapa kuimarisha timu hii.
“Tuliwatenga wachezaji ambao tunanuia kukopesha vilabu vingine lakini orodha hii haifuatiliwi kwa maanani.
Nia yangu ni Leopards wasonge mbele katika mkondo wa pili kwa hivyo, mambo ni lazima yatekelezwe kwa njia mwafaka. Hadi sasa, hatuna uwanja unaofaa kwa mazoezi na hili tatizo bado halijasuluhishwa,” aliendelea kufoka.
Alidokeza kuwa amepata nafasi zingine za kuendeleza kazi yake huku akitoa makataa atajiuzulu iwapo malalamishi yake hayatasikizwa.
“Najihisi nyumbani hapa AFC na ninanuia kuendelea kazi hapa lakini nitatafakari mengine iwapo hatua haitachukuliwa kutatua shida za maadili tulizo nazo. Nimepata fursa nyingine za ajira kutoka vilabu mbalimbali,” kocha huyo aliyeondoka Ijumaa kwa likizo ndogo Ubelgiji alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment