Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 February 2017
Friday, February 03, 2017

WENGER AMTOLEA MACHO THIERRY HENRY 'MPYA'


Na FLORENCE GR

Kwa kile kinachoonekana kama kutaka kumsajili katika kikosi chake kocha wa Arsenal amekiambia kituo cha television cha  Ligue 1 kuwa amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana mchezaji kinda wa As Monaco Kylian Mbappe huku akisema mchezaji huyo anaweza kuwa Thierry Henry mpya.

Mbappe mwenye umri wa maika 18 amekuwa akifananishwa na mshambuliaji wa zamani wa ufaransa na Arsenal Thierry Henry ambae alianza kucheza soka kwenye timu ya vijana ya Stade Louis II kutokana na kasi , uwezo wa kukokota mipira na uwezo wa kufunga aliokuwa nao mchezaji huyo.

Mchezaji huyo alifanikiwa kuvunja rekodi ya Henry na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo aliyefanikiwa kuifungia Monaco pale alipofunga goli dhidi ya Troyes mwezi  wa February mwaka jana alipokuwa na umri wa miaka 17 miezi miwili na siku moja.

Akimuongelea mchezaji huyo 'Mbappe sio Thierry Henry halisi lakini anasifa zinazofanana nae' alisema Wenger.

'Anakipaji kama alichokuwa nacho Henry baada ya hapo, je anamotisha ,hamu na akili kama alizokuwazo Thierry Henry? miaka miwili ijayo itatuambia lakini dalili za kwanza zinavutia sana'.

Wenger aliongeza kuwa 'tunamfatilia, tunamjua vizuri sana na anaendelea vizuri. Nafikiri ameongeza mkataba na Monaco kwahiyo ni Monaco ndio wenye uamuzi wa kuamua mustakabali wake'.

Alipoulizwa kuhusu kamawalishafanya jitihata za kutaka kumsajili mchezaji huyo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi dhidi ya Chelsea, wenger alisema kuwa 'msimu ujao tulipeleka ofa ya kutaka kumsajili lakini aliamua kubaki hapo alipo sasa hivi'.

Monaco walimuongeza mkataba wa miaka miatatu msimu uliopita paata ya kudaiwa Arsenal kuanza kumnyemelea nyota huyo, kwa upande mwingine Mbappe amefichua kuwa alikataa kujiunga na timu za Real Madrid na PSG kwa sababu anataka kuendelea kubaki Monaco kwani ndio iliyomkuza kipaji chake .


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!