Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 February 2015
Monday, February 16, 2015

DRFA YAWAPONGEZA AZAM NA YANGA,MICHUANO YA VILABU AFRIKA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                     Release N0.06
Februari,16/2015

Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya vilabu barani afrika klabu ya Azam FC na Yanga SC,kwa kuanza na ushindi katika mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.

Yanga walikuwa wa kwanza kuwapa raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini,baada ya kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa Polisi toka Botswana BDF 11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe la shirikisho.

Kwa upande wa Azam FC,wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Didier Kavumbagu pamoja na John Rafael Bocco,katika mchezo wa kuwania kombe la klabu bingwa uliopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi.

Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo nzuri waliyoanza nayo,na kusema kuwa maandalizi yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea mashindano hayo ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na makocha,ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.

Kasongo,pia amesema DRFA imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa Dar es salaam na maeneo mengine nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hizo mbili,na kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya licha ya dosari ndogo ndogo zilizojitokeza.MICHUANO YA LIGI YA MKOA DAR INAENDELEA.

Michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam inaendelea tena wiki hii kwa timu 8 kushuka katika viwanja tofauti,kupambana ili kuusaka ubingwa huo pamoja na kupata nafasi ya kuingia katika ligi daraja la pili taifa.

Mechi za leo Februari 16,2015/Azania Ngano watakipiga dhidi ya Yanga U20 (Katika uwanja wa Karume),Stakishari watacheza na FFU (uwanja wa B.Mkapa),Changanyikeni wataumana dhidi ya Tuamoyo (uwanja wa MWL/Nyerere) na New Kunduchi wataoneshana kazi dhidi ya Sinza Stars (uwanja wa Kines).

Kivumbi hicho kitaendelea tena kesho Kutwa Februari 18,2015 kwa Simba U20 kucheza na Ukonga UTD (Uwanja wa karume),Red Coast watacheza dhidi ya Shababi (MWL/Nyerere),Zakhem watacheza na Sifa UTD ( Uwanja wa Bandari) na Beirahotspurs watakipiga dhidi ya Pan African (uwanja wa Kines).

IMETOLEWA NA DRFA
OMARY KATANGA

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano DRFA

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!