Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 February 2015
Saturday, February 14, 2015

Lugha ya kiingereza yaleta utata ndani ya Arsenal.


Na Oscar Oscar Jr

Lugha ya Kiingereza kumbe sio huku kwetu tu, hata Uingereza nako ni tatizo. Kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amezungumza kuwa kitendo cha mlizi wake wa kati, Gabriel Paulista kutofahamu lugha ya kiingereza hata kidogo inaweza kuigharimu timu hiyo kufungwa magoli.

Wenger amesema Paulista anapaswa kufahamu baadhi ya maneno ya kiingereza ili aweze kuwasiliana na wachezaji wenzie uwanjani. 

Paulista ambaye amesajili kwenye dirisha dogo akitokea kwenye klabu ya Villareal ya nchini Hispania, ameripotiwa kutofahamu hata kidogo lugha ya kiingereza na hivyo kukosa mawasiliano na baadhi ya wachezaji wenzie.

Wakati Arsenal wakijiandaa kuwavaa Middlesbrough kwenye mchuano wa kombe la FA, Paulista ametajwa kuwa ataanza kwenye kikosi hicho cha Gunners huku Per Mertesacke akitajwa kupumzishwa. 

Wenger amesema mchezaji huyo anapaswa kujua japo maneno machache kama refa, nenda mbele, kuotea, kaba n.k ili iwe rahisi kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Kwa upande mwingine Wenger amesema kutofahamu lugha napo kunafaida yake kwa sababu mchezaji anaepuka presha za vyombo vya habari na kujikiti kwenye kucheza tu kwa sababu kitakachokuwa kinazungumzwa na wachambuzi hatokuwa anakielewa na hivyo hatokuwa na presha yoyote.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!