Searching...
Image and video hosting by TinyPic
17 February 2015
Tuesday, February 17, 2015

MAHUNDI, BAHANUZI WACHEZAJI BORA VPL


Kiungo wa timu ya Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Disemba 2014 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.
Aidha mshambuliaji wa timu ya Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi mzunguko wa 15 kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Bahanuzi anayechezea timu ya Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na mchango mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini.
Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!