Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 January 2015
Wednesday, January 07, 2015

Uwanja wa Kaitaba sasa ni kama Ulaya.


Na Florence George

Moja kati ya maeneo ambayo Uongozi wa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania, Jamal Malinzi ulionyesha nia ya kufanyia marekebisho mara tu walipoingia madarakani, ilikuwa ni viwanja vinavyotumika kwenye ligi kuu Tanzania bara. 

Hatu ya kwanza Uongozi huo uliyochukuwa, ilikuwa ni kuvifungia viwanja vingi msimu uliopita ambavyo havikuwa na hali nzuri na Uwanja wa Kaitaba ulikuwa miongoni vya vilivyofungiwa kuuimika kwa mechi za ligi kuu.

Habari zilizopo ni kwamba, Uwanja wa Kaitaba wa mkoani Kagera utaanza kuwekwa nyasi bandi kuanzia tarehe 13 ya mwezi huu na mechi zote ambazo zilipangwa kuchezwa kwenye dimba hilo zitahamishiwa mahali pengine kwa muda.

Ukarabati wa Uwanja huo unafadhiliwa na mpango wa FIFA wa kusaidia maendeleo ya soka la Tanzania. Mpaka sasa viwanja vya Amani Zanzibar, Uwanja wa Karume Dar es Salaam na ule wa Uhuru tayari vimenufaika na Mpango huo.

Kama mpango wa kuweka nyasi bandia kwenye viwanja utakuja kufika mahali kote nchini, itakuwa msaada mkubwa sana. Tayari msimu huu, Mechi mbili zimeahirishwa kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro kutokana na Mvua zilizopelekea Uwanja kujaa maji.

Mchezo kati ya Mtibwa Sugar uliwahi kuahirishwa na kuchezwa siku iliyofuata wakati timu hizo zikitoka sare ya 1-1 na hali kama hiyo pia, ilijitokeza kwenye mchezo baina ya Mtibwa Sugar na Stand United. Kama Uwanja huu utapata miundombinu ya kisasa, matatizo hayo yanaweza kuepukwa.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!