Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 January 2015
Monday, January 19, 2015

Xavi awataka Silva na Carzola Barcelona.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa Barcelona Xavi Hernandez ameonyesha kufurahishwa na viungo washambuliaji wa timu za Manchester City na Arsenal kutoka nchini Hispania David Silva na Santi Carzola na angetamani kucheza nao kwenye klabu ya Barcelona.

Viungo hao wawili ambao wameonyesha viwango vizuri kwenye ligi kuu nchini Uingereza ambapo Silva amehusika kwenye magoli nane ya Manchester City msimu huu kwa kufunga magoli sita na kutoa pasi mbili (assist) za magoli huku Carzola akihusika kwenye magoli tisa kwa kufunga magoli matano na kutoa pasi nne za magoli (assist).

Xavi mwenye umri wa miaka 34 alipoulizwa ni wachezaji gani angependa kuwasajili kwaajili ya Barcelona alijibu “Silva (na) Carzola… kuna vipaji vizuri kwasasa kwenye soka la Hispania ambavyo ningependa kuvisajili kwaajili ya Barcelona”.

Xavi ambaye anaweza kucheza dhidi ya Silva kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya mapema mwezi Februari kwenye mchezo kati ya Manchester City dhidi ya Barcelona akiongelea mchezo huo alisema “michezo yote ni migumu, mecho yetu dhidi ya Manchester City itakuwa ngumu sana”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!