Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 January 2015
Monday, January 19, 2015

Mats Hummels haendi kokote.


Na Chikoti Cico

Nahodha na beki wa timu ya Borrusia Dortmund Mats Hummels ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kuhamia klabu mbalimbali za ligi kuu nchini Uingereza zikwemo klabu za Arsenal na Manchester United akiongea na gazeti moja nchini Ujerumani amekataa kuiacha klabu ya Dortmund.

Hummels ambaye alisajiliwa mwaka 2009 na klabu ya Dortmund akitokea Bayern Munich amesisitiza kwamba pamoja na kusuasua kwa klabu yake hiyo ambayo iko kwenye hatari ya kushuka daraja huku pia kukiwa na uwezekano wa kushindwa kupata nafasi ya kushiriki klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao bado hataondoka.

Akiongea na gazeti la Die Welt la nchini Ujerumani alisema “fununu zote hizo ni swala jingine, sijawahi kusema chochote kuhusu hayo. Nilifanya hivyo zamani na ntaendelea kufanya hivyo. (Ulaya) sio jambo la kiuhalisia tena, kupigana kwaajili ya ligi ya mabingwa halipo kwenye kichwa changu”.

Aliendelea kusema “kimsingi sihitaji kucheza ligi ya mabingwa ili niwe na furaha, labda tutapoteza wachezaji kwa kushindwa kuingia kwenye ligi ya mabingwa lakini ninachoweza kukwambia ni kwamba tusipopoteza wachezaji 15 kwa mara moja tutakuwa timu bora msimu ujao”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!