Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 January 2015
Friday, January 16, 2015

Uchambuzi: Swansea vs Chelsea



Na Chikoti Cico

Ligi kuu nchini Uingereza itaendelea kushika kasi tena mwishoni mwa juma hili huku Libert stadium wenyeji Swansea City wataikaribisha timu ya Chelsea katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utakaochezwa siku ya Jumamosi saa 12 kamili jioni.

Katika mchezo huo timu ya Swansea ambayo inashika nafasi ya tisa ikiwa na alama 30 kwenye msimamo wa ligi itaanza maisha mapya bila ya mshambuliaji wake Wilfried Bony ambaye tayari amesajiliwa na Manchester City hivyo Befitimbi Gomis anatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Kocha wa Swansea Gary Monk kwenye mchezo huyo atawakosa viungo Jonjo Shelvey ambaye anamalizia adhabu ya kufungiwa mechi nne huku Ki Sung-Yueng akiwa kwenye kombe la Asia akiiwakilisha timu ya taifa ya Korea ya Kusini.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Swansea wamefungwa michezo mitano na kutoka sare michezo miwili katika michezo saba waliyocheza na Chelsea kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Kikosi cha kocha Monk kinaweza kuwa hivi: Fabianski, Rangel, Fernandez, Williams, Taylor, Britton, Carroll, Routledge, Dyer, Sigurdsson, Gomis.

Nayo klabu ya Chelsea inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 49 inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho kwenye mchezo huo atamkosa beki wa kulia Cesar Azpilicueta ambaye anasumbuliwa na mtoki huku kipa Thibaus Courtois ambaye alikosekana kwenye mechi mbili zilizopita baada ya kuumia kidole cha mkono akitarajiwa kurejea golini.

Kwa upande wa Chelsea takwimu zinaonyesha katika michezo mitano ya ugenini iliyopita kwenye ligi Chelsea imeshinda mchezo mmoja na kufungwa michezo miwili huku ikitoka sare michezo michezo miwili.

Kikosi cha kocha Mourinho kinaweza kuwa hivi: Courtois, Ivanovic, Luis, Cahill, Terry, Fabregas, Matic, Oscar, Willian, Hazard,Costa


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!