Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 January 2015
Friday, January 16, 2015

Manuel Pellegrini kocha bora Desemba.
Na Chikoti Cico

Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya kocha bora kwa mwezi Desemba kwenye ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuiongoza Man City kushinda michezo mitano ndani ya mwezi huo.

Timu ya Manchester City ambayo ilijikusanyia alama 16 kati ya alama 18 kwenye mwezi wa Desemba bila ya kupoteza mchezo hata mmoj ilishinda michezo mitatu ugenini dhidi ya Sunderland, Leicester na West Brom na pia kuzifunga Everton na Crystal Palace nyumbani Etihad huku ikitoka sare dhidi ya Burnley ndani ya mwezi huo.

Pamoja na kuweza kujikusanyia alama 16 lakini pia ni mwezi ambao kocha wa City aliandamwa na wachezaji wengi majeruhi wakiwemo washambuliaji wake watatu Sergio Aguero, Stevan Jovetic na Edin Dzeko pia nahodha Vicent Kompany lakini walifanikiwa kufunga jumla ya magoli 14 katika michezo sita waliyocheza ndani ya mwezi Desemba.

Hii ni mara ya tatu kwa Pellegrini kunyakua tuzo ya kocha bora wa mwezi ndani ya miezi 18 aliyoifundisha Man City na aliwahi kuchukua tuzo hiyo mara mbili mfululizo kwa mwezi Desemba 2013 na Januari 2014.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!