Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 January 2015
Friday, January 16, 2015

Uchambuzi: Aston Villa vs Liverpool


Na Chikoti Cico

Nyasi za uwanja wa Villa Park zitawaka moto wikendi hii kwa mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza kati ya wenyeji timu ya Aston Villa dhidi ya Liverpool. Mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi saa 12 jioni.

Aston Villa ambayo inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 22 inahitaji kushinda mchezo huo dhidi ya Liverpool na kuchukua alama zote tatu muhimu baada ya kuwa na matokeo mabovu kwa mechi nyingi zilizopita.

Kocha wa Aston Villa Paul Lambert ambaye yuko hatarini kufukuzwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo, kwenye mchezo huo atawakosa Ciaran Claran ambaye amesimamishwa mchezo mmoja pia atawakosa Ron Vlaar, Philippe Senderos na Libor Kozak ambao ni majeruhi.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha katika michezo minane iliyopita ya ligi kwenye uwanja wa Villa Park timu ya Aston Villa imeshinda mchezo mmoja na kufungwa michezo mitatu huku wakitoka sare michache minne.

Pia takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa klabu hiyo Christian Benteke amefunga magoli manne katika michezo minne dhidi ya Liverpool.

Kikosi cha QPR kinaweza kuwa hivi: Guzan; Hutton, Okore, Baker, Cissokho; Westwood, Cleverley, Delph; Agbonlahor, Benteke, Weimann

Kwa upande wa timu ya Liverpool ambayo mpaka sasa inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 32 kwenye msimamo wa ligi inatarajiwa kuingia kwa nguvu kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufikia nafasi nne za juu (top four)

Nahodha na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard pamoja na Adam Lallana wana nafasi ya kurejea uwanjani kwenye mchezo huo baada ya kuwa majeruhi huku Gerrard akitolewa nje wakati wa mapumziko kwenye mchezo uliopita dhidi ya Sunderland kutokana na kukaza kwa ukano wa uvungu wa goti huku Lallana akirejea mapema zaidi baada ya kuumia wakati wa mchezo wa mwaka mpya.

Kwa upande wa Liverpool takwimu zinaonyesha katika michezo 16 iliyopita ya ligi kwenye uwanja wa Villa Park imeshinda michezo 10 na kufungwa mchezo mmoja huku ikitoka sare michezo mitano pia takwimu zinaonyesha nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amefunga magoli mengi dhidi ya Aston Villa kuliko klabu nyingine yoyote, magoli 12.

Kikosi cha kocha wa Liverpool Brendan Rodgers kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Can, Skrtel, Sakho; Manquillo, Henderson, Lucas, Moreno; Coutinho, Markovic, Sterling

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!