Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 January 2015
Saturday, January 31, 2015

Uchambuzi: Arsenal vs Aston Villa


Na Chikoti Cico

Kwenye uwanja wa Emirates wikendi hii timu ya Arsenal itaikaribisha timu ya Aston Villa katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza mchezo utaka
opigwa leo.
Timu ya Arsenal ambayo inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza ikiwa na alama 39 inatarajiwa kucheza kwa nguvu zote katika kutafuta ushindi kwenye mchezo huo ili kujitengeneza mazingira mazuri ya kushika kati ya nafasi nne za juu (top four).
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwenye mchezo huo atawakosa Jack Wilshere, Mikel Arteta, Abou Diaby na Mathieu Debuchy ambao ni majeruhi huku Danny Welbeck ambaye anakarabia kurejea uwanjani baada ya kuwa nje kutokana na kuwa majeruhi naye hatacheza mchezo huo.
Mshambuliaji wa timu hiyo Alex Sanchez ana hatihati ya kutokucheza mchezo huo kutokana na majeraha ya ukano wa mvungu wa goti huku beki aliyesajiliwa wiki hii kutoka Villarreal Gabriel Paulista akitarajia kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza mchezo huo.
Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud amefunga magoli matano katika michezo minne iliyopita ya ligi pia takwimu zinaonyesha klabu ya Arsenal haijashinda michezo mitatu mfululizo ya ligi toka kuanza kwa msimu huu.
Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Ospina; Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal; Coquelin, Ramsey, Cazorla; Walcott, Giroud, Ozil
Nayo klabu ya Aston Villa ambayo inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 22 inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo na kucheza kufa na kupona ili kupata ushindi na kuondokana na balaa la kushuka chini zaidi kwenye msimamo wa ligi.
Kocha wa Aston Villa Paul Lambert kwenye mchezo huo atawakosa walinzi Ron Vlaar na Philippe Senderos ambao ni majeruhi pia Joe Cole atakosekana kwenye mchezo huo huku mshambuliaji Gabriel Agbonlahor ambaye alikuwa majeruhi akitarajiwa kurejea kikosini.
Aston Villa kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa klabu hiyo Christian Benteke amefunga magoli matatu katika michezo minne iliyopita ya ligi dhidi ya Arsenal pia takwimu zinaonyesha Villa haijafunga goli lolote katika michezo mitano iliyopita huku wakiwa wakijikusanyia alama tatu tu katika michezo saba iliyopita ya ligi.
Kikosi cha Aston Villa kinaweza kuwa hivi: Guzan; Hutton, Okore, Baker, Cissokho; Gil, Westwood, Delph, Cleverley; Agbonlahor, Benteke

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!