Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 January 2015
Sunday, January 25, 2015

SIMBA VS AZAM NI KIVUMBI NA JASHO






Na Samuel Samuel
0652464525

Toka Azam FC wapande chati kwenye ligi kuu Tanzania bara , wamekuwa wana matokeo mazuri dhidi ya Simba SC. Azam FC inakutana na Simba SC leo ikiwa na pointi 20 kileleni mwa ligi wakati wekundu wa Msimbazi Simba wapo nafasi ya tisa wakiwa na pointi 12 tu katika mechi tisa alizocheza.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana mwaka jana kwenye ligi na Azam FC kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja huku goli la Simba SC likitiwa kwenye kamba na beki kisiki Joseph Owino.

Lakini kama ilivyokuwa msimu uliopita , ukitazama msimamo wa ligi matokeo ya timu hizi yanasubiriwa kwa hamu kubwa na mahasimu wao wakubwa Yanga.

Kuna kila dalili mashabiki wa Yanga kuitakia mema Simba kinafiki tu kwenye mchezo wa leo ili Azam FC isitengeneze gap kubwa na Yanga ambao jana walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polis Moro.

Leo nyasi za Uwanja wa Taifa zitawaka moto tukishuhudia vita ya viungo mahili kwenye ligi kwa sasa. Ukiitazama Azam FC pale kati kuna Bolou Michael, Mudathir Yahya na Frank Domayo aliyewalaza na viatu Kagera Sugar mechi iliyopita pale Mwanza.

Viungo hao wote wana uwezo mkubwa wa kutawala kiungo lakini ukimtazama Domayo na Balou ni mafundi hasa wa pasi ndefu za mwisho kwa strikers waroho kama Didier Kavumbagu na Kipre Tche Tche.

Utamu zaidi ni jinsi Pascal Wawa anavyozidi kuimarika kama mlinzi wa kati kwa kusaidiana na kiungo kuanzisha mashambulizi na kuwakataa mafowadi kushambulia kupitia kati .

Dany Sserunkuma na Elias Maguli wana kazi ya ziada kupenya ngome ya Azam FC. Murshid pamoja na Tshabalala wapo vizuri kwenye marking lakini wanahitaji umakini mkubwa kuwazuia mawinga wenye kasi na maamuzi ya haraka kama Brian Majwega .

Kama kuna usajili Azam FC wamelamba dume ni kwa huyu winga. Ana uwezo mkubwa sana kuchezesha strikers na kumiliki mpira kwa kuipanga timu kuandaa shambulio zuri kutokea pembeni.

Simba mechi ya kesho wanaingia uwanjani wakiwa vizuri kisaikolojia kutokana na ushindi uliopita dhidi ya Ndanda na kombe la Mapinduzi kabatini linazidi kuwapa morali kuwavaa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu.

Kuanza kufunga kwa Dany Sserunkuma kunaongeza hamasa ya ushindi. Mimi naiona ni kama mechi ya viungo zaidi maana wote wana viungo bora kubadilisha matokeo wakati wowote.

Huku Said Ndemla, Mkude na Okwi kule Domayo, Balou , Majwega na mchawi Mudathir.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!