Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 January 2015
Saturday, January 24, 2015

Kundi D AFCON bado sana.
Na Chikoti Cico

Kundi D kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika mpaka sasa bado bichi kabisa baada ya kila timu kwenye kundi hilo kujikusanyia alama 2 kabla ya michezo ya mwisho ya kundi hilo itakayopigwa wiki ijayo Jumatano.

Katika mchezo ya kundi hilo uliyochezwa leo kwenye uwanja wa Estadio de Malabo timu ya taifa ya Ivory Coast imetoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Mali, katika mchezo huo uliowakutanisha vigogo hao wa Afrika Mali ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya sita ya mchezo kupitia kwa Bakary Sako.

Na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Mali walitoka kifua mbele wakiwa wanaongoza kwa goli hilo moja, kipindi cha pili kilianza kwa Ivory Coast kutafuta goli la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Wilifried Bony bila mafanikio.

Huku mchezo ukikaribia kuisha na Mali wakiamini kuchukua alama zote tatu alikuwa ni Max Gradel aliyeisawazishia Ivory Coast kwenye dakika ya 86 ya mchezo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Serge Aurier kabla ya kuachia shuti kali kwa mguu wa kushoto lililokwenda wavuni na kuamsha kelele za mashabiki uwanjani hapo.

Mpaka mwisho wa mchezo huo timu zote mbili ziligawana alama moja moja na kuendelea kulifanya kundi D kushindwa kutabirika hivyo swali la kwamba timu gani itavuka hatua ya makundi kutoka kwenye kundi hilo litajibiwa siku ya Jumatano tarehe 28 Januari kwa michezo ya mwisho.

Mchezo mwingine wa kundi D uliopigwa kwenye uwanja wa Estadio de Malabo ulikuwa ni kati ya Cameroon dhidi ya Guinea, mchezo ambao pia uliisha kwa sare ya goli 1-1, ambapo Cameroon ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 13 kupitia kwa Max Gradel kabla ya Ibrahima Traore kuisawazishia Guinea kwenye dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza.

Kutokana na kwamba kila timu imejikusanyia alama mbili kwenye msimamo wa kundi D mpaka sasa, hivyo kwenye michezo wa mwisho ya kundi hilo itakayopigwa siku ya Jumatano ya wiki ijayo timu yoyote itakayoshinda itakuwa imevuka hatua ya makundi na kuingia hatua ya robo fainali.

Kwenye michezo ya mwisho Ivory Coast itacheza dhidi ya Cameroon huku Mali wakicheza dhidi ya Guinea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!