Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 January 2015
Sunday, January 18, 2015

Ronaldo atupia tena ,Real Madrid Haikamatiki




Na Florence George


Klabu ya soka ya Real Madrid ya nchini Hispania imeongeza tafauti ya pointi dhidi ya mahasimu wake wa karibu klabu ya Fc Barcelona na kufika pointi nne mara baada ya kuifunga timu ya Getafe magoli 3-0 katika mechi iliyochezwa leo mchana.


Haikuwa kazi rahisi kwa mabingwa hao wa Ulaya ambao wameanza vibaya mwaka 2015 mara baada ya kutolewa katika kombe la Mfalme na Atletico Madrid siku ya Alhamisi na kwa mara ya kwanza Real Madrid wameshindwa kufunga goli katika kipindi cha kwanza msimu huu dhidi ya Getafe.

Mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2014 Cristiano Ronaldo ndie aliyekuwa wa kwanza kuifungia timu yake goli katika dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mfaransa Karim Benzema.

Mshambuliaji kutoka Wales, Gareth Bale aliongeza goli la pili dakika nne baadae  kabla ya Ronaldo kufunga tena dakika 11 kabla ya mchezo kumalizika na kufikisha magoli 28 katika michezo 17 aliyocheza msimu huu.

Real madrid imefikisha pointi45 katika mechi 18 iliyocheza  ikiwa na mechi moja mkononi,huku Fc Barcelona ikiwa na pointi 41 katika mechi 18 ipo nafasi ya pili na inajiandaa kumenyana na
Deportivo La Coruna baadae leo hii.

Valencia na mabingwa watetezi Atletico Madrid ambao watakuwa wenyeji dhidi ya Granada iliyo nafasi ya 20 wanalingana pointi ,alama 38 kila moja huku Valencia ikiwa juu kwa tofauti ya magoli mara baada ya kushinda magoli 3-2 dhidi ya Almería hapo jana.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!