Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 January 2015
Sunday, January 18, 2015

Olympique Lyon yajikita kileleni wa ligi kuu nchini Ufaransa.





Na Florence George

Klabu ya soka ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa imefanikiwa kuongeza tofauti ya pointi na kufikisha pointi nne kileleni dhidi ya Olympique de Marseille iliyokatika nafasi ya pili mara baada ya kuifunga timu ya RC Lens magoli 2-0 katika muendelezo wa mechi za ligi kuu nchini Ufaransa.


Staa wa timu hiyo Alexandre Lacazette alifikisha goli lake la 12 katika ligi mara baada ya kuifungia timu yake goli la pili na kuihakikishia timu yake ushindi ambapo sasa imefikisha pointi 45 katika michezo 21 iliyocheza mpaka sasa.

Olympique de Marseille iliyokatika nafasi ya pili itashuka dimbani leo kupambana na timu ya En Avant Guingamp na kama wakifanikiwa kushinda watapunguza tofauti ya pointi na kubakia moja dhidi ya vinara wa ligi hiyo.

St Etienne walio katika nafasi ya tatu,pointi sita nyuma ya vinara watasafiri kuwafuata timu ya Stade Rennais iliyokatika nafasi ya tisa ,huku PSG iliyokatika nafasi ya nne watakuwa wenyeji wa Evian Thonon Gaillard. 

Ezequiel Lavezzi na Edinson Cavani, watarudi uwanjani mara baada ya kuachwa na kocha Laurent Blanc katika michezo mitatu iliyopita mara baada ya kuchelewa kuripoti kambini baada ya mapumziko ya mwezi December.

Sasa Lyon wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 45,wakifuatiwa na  Marseille yenye pointi 41 huku St Etienne wakiwa na ponti 39 na PSG kufunga orodha ya timu nne za juu ikiwa na pointi 38.






 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!