Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 January 2015
Thursday, January 15, 2015

Real Madrid yatupwa nje Copa del Rey.


Na Chikoti Cico

Magoli mawili yaliyofungwa na Fernando Torres ndiyo Fernando Torres yalisaidia kuitupa nje ya kombe la Mfalme yaani Copa del Rey klabu ya Real Madrid huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza Torres anaifunga Real Madrid akiwa anaichezea Atletico Madrid.

Baada ya mchezo wa kwanza kwenye uwanja wa Vicente Calderoni nyumbani kwa Atletico kuisha kwa wenyeji kushinda kwa magoli 2-0, mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu ulishuhudia Torres akifunga magoli mawili kwenye dakika ya kwanza na 46 na kuipa Real Madrid mlima wa kupanda ili kushinda mchezo huo.

Nao Madrid waliweza kupata magoli mawili kupitia kwa Ramos kwenye dakika ya 20 na Ronaldo kwenye dakika ya 54 na kufanya matokeo mpaka mwisho wa mchezo huo kuwa 2-2 hivyo Atletico kuitupa nje Real Madrid kwa jumla ya magoli 4-2 na kuingia hatua ya robo fainali ambapo watacheza na Barcelona.

Kabla ya mchezo huo kuanza Christiano Ronaldo alionyesha tuzo ya Ballon d’Or aliyonyakua siku ya Jumatatu kwa mashabiki wa Real Madrid huku pia Toni Kroos, Sergio Ramos na James Rodriguez nao wakionyesha tuzo zao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!