Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 January 2015
Thursday, January 15, 2015

Mourinho ni kocha wa karne


Na Chikoti Cico

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho atwaa tuzo ya kocha bora wa karne nchini Ureno, tuzo hiyo ilitolewa wakati shirikisho la soka nchini Ureno likisheherekea jubilei ya miaka 100 ya kusimamia soka la nchini humo.

Kocha huyo ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Porto, Inter Milan, Real Madrid na Chelsea kwa mara ya kwanza mwaka 2004-2007 kabla ya kurejea tena mwaka 2013 kuifundisha klabu hiyo kutoka jiji la London mpaka sasa amechukua tuzo hiyo baada ya kuiwakilisha vyema nchi ya Ureno wakati akizifundisha klabu hizo.

Mourinho mwenye umri wa miaka 51 amefanikiwa kuchukua makombe ya ligi zote alizofundisha nchini Ureno alifanikiwa kunyakua kombe la ligi mara mbili na Porto pia huku pia nchini Uingereza alifanikiwa kunyakua kombe la ligi mara mbili na Chelsea, nchini Italia alinyakua kombe la ligi ya Serie A na Inter Milan na pia alinyakua la liga akiwa na Real Madrid.

Kocha huyo maarufu kwa kuwa na maneno mengi pia alifanikiwa kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Ulaya (Uefa Champions League) mara mbili wakati akizifundisha klabu za Porto na Inter Milan.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!