Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Blind amjibu Gary Neville.


Na Chikoti Cico

Kiungo mkabaji wa klabu ya Manchester United, Daley Blind amjibu beki na nahodha wa zamani klabu hiyo Gary Neville ambaye aliwahi kusema kwamba “Blind anacheza pasi nyingi mraba na anachukua maamuzi marahisi” Neville ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka aliyasema hayo akiwa kwenye studio za televisheni ya Sky Sport.

Blind ambaye alisajiliwa na United akitokea klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi alipoulizwa kuhusu maneno hayo ya Gary Neville alisema “ni kweli huwa namsikiliza lakini najaribu kucheza mchezo wangu na kufanya kile kocha anachotaka kutoka kwangu na ni kumiliki mpira, mara kwa mara kuna mtu ambaye hutaka kusema kitu kuhusu kocha ama timu vinginevyo kusingekuwa na mvuto wa televisheni”.

“Ninaweza kuchukua kukosolewa kidogo, watu wa televisheni wanaweza kusema wanachotaka unaskia lakini nafikiri nimecheza kiasi vizuri. Ni kweli mara chache unaweza kucheza mipira mbele lakini wakati mwingine ni vema kumiliki mpira na kuwafanya wachezaji wenzako wacheze vizuri”.

Aliendelea kusema “ninaweza kuwafanya wachezaji wengine muhimu zaidi kuliko mimi, kama ninaweza kufanya hivyo kwa kubadilisha mchezo kwa upande mwingine ama kusubiri wakati muafaka kufanya hivyo basi nitafanya.

Kama kuna nafasi mbele basi nitacheza mpira huo lakini wakati mwingine nafikiri ni vema kumiliki mpira kubadilisha upande kwa upande na kuhamisha mpira na kutafuta wachezaji ambao wanawezas kufanya vitendo binafsi mimi sio mchezaji wa kufanya hivyo, napenda mchezo wa kumiliki mpira na kukaa na mpira”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!