Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

EPL yatisha kwa pesa duniani.




Na Chikoti Cico

Ligi kuu nchini Uingereza (EPL) yatisha kwenye orodha ya klabu 40 tajiri duniani iliyotolewa siku ya Alhamisi na “Accountants Deloitte”, timu zote 20 za ligi kuu nchini Uingereza kwa msimu uliopita zimeingia kwenye orodha hiyo huku hata timu ya Norwich City iliyoshuka daraja msimu uliopita ikiingia kwenye orodha hiyo.

Klabu tano kutoka ligi kuu nchini Uingereza zimeingia kati ya timu 10 za juu kwenye orodha hiyo huku klabu ya Manchester United ikishika nafasi ya pili nyuma ya Real Madrid.

United waliingiza kipato cha pauni milioni 433 kwenye msimu wa 2013-2014 huku Madrid wakiingiza kipato cha pauni milioni 459.

Bayern Munich wanashika nafasi ya tatu kwa kiasi cha pauni milioni 407.7. Barcelona wako nafasi ya nne kwa kiasi cha pauni milioni 405.3 na PSG nafasi ya tano kiasi cha pauni milioni 396.6.

Manchester City wanshika nafasi ya sita wakiwa na kiasi cha pauni milioni 346.5, Chelsea nafasi ya saba pauni milioni 324.4, Arsenal nafasi ya nane pauni milioni 300 na Liverpool nafasi ya tisa pauni milioni 255.8.

Klabu za ligi kuu nchini Uingereza zimeingiza pesa nyingi kupitia mikataba mipya ya televisheni 2013-2016 ambapo kuanzia msimu uliopita ziliingizia klabu nyingi za Uingereza mapato mengi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!