Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 January 2015
Sunday, January 25, 2015

Olympique Lyon ya Alexandre Lacazette ni Hatarii ligi kuu Ufaransa.





Na Florence George


Klabu ya soka ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa imezidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu nchini Ufaransa mara baada  ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Metz mchezo uliochezwa mapema hii leo.

Mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Alexandre Lacazette ndiye alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake dakika ya 31 kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Metz, Guido Milan  kufanya faulo ndani eneo la hatari na kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Alexandre Lacazette mwenye umri wa miaka 21 ambaye hadi sasa anaongoza kwa kufunga magoli mengi kweneye ligi hiyo (21), hakuweza kuendelea na mchezo huo baada ya kuumia dakika ya 33 na nafasi yake kuchukuliwa na Maxwell Cornet.

Kiungo Corentin Tolissoalihakikishia timu yake ushindi mara baada ya kufunga goli la pili katika dakika za mwishoni mwa mchezo huo.

Kwa matokeo hayo yanawafanya Olympique Lyon kufikisha pointi 48 katika michezo 22 pointi nne zaidi ya Olympique de Marseille amabo walifungwa magoli 2-1 dhidi ya Nice siku ya Ijumaa.

Mabingwa watetezi walio katika nafasi ya tatu timu ya PSG watasafiri kuwafuata St Etienne walio nafasi ya nne na endapo vijana hao wa Laurent Banc watashinda watalingana pointi na Marseille.



 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!