Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 January 2015
Sunday, January 25, 2015

Arsenal yasajili Mbrazili


Na Chikoti Cico


Wakati dirisha dogo la usajili likikaribia kufikia tamati, klabu ya Arsenal imefanikiwa kunasa saini ya mlinzi wa Villarreal Mbrazili Gabriel Paulista kwa ada ya pauni milioni 15.

Kwa upande wa pili, mshambuliaji wa Arsenal, Joel Campbell akijiunga kwa mkopo na klabu hiyo kutoka Hispania mpaka mwisho wa msimu huu kama sehemu ya makubaliano kati ya timu hizo mbili.

Taarifa za kukamilika kwa dili la kumsajili Paulista zimekuja baada ya beki huyo kuachwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 wa Villarreal kilichocheza dhidi ya Levante usiku wa Jumamosi katika mfululizo wa mechi za la liga.

Klabu ya Villarreal ilithibitisha usajili wa beki huyo kupitia ukurasa wao wa Twitter kwa kuandika “taratibu za makubaliano kwaajili ya uhamisho wa Gabriel na @Arsenal umekamilika.

Atasema kwaheri leo kabla ya tafrija. Kila la kheri”. “Karibu @Joel_campbell12 Villareal kwa Arsenal kukubali kumtoa kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu”.

Pamoja na kukamilika kwa usajili wa beki huyo lakini Arsenal wanaweza kukutana na changamoto ya kibali cha kufanya kazi kwaajili ya mchezaji huyo ambaye mpaka sasa hajacheza michezo ya kimataifa ingawa Arsenal wataweza kukata rufaa kwa maamuzi yoyote yatakayofanyika kumyima Paulista kibali.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!