Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 January 2015
Thursday, January 15, 2015

Bony amfukuza Jovetic Manchester City


Na Chikoti Cico

Usajili wa mshambuliaji mpya wa Machester City Wilifried Bony kutoka Swansea City kwa ada ya pauni milioni 25 huku akitarajiwa kuchukua mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki umesababisha nafasi ya Stevan Jovetic kwenye kikosi cha Manchester City kuwa hatarini hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Usajili huo wa Bony umesababisha idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye kikosi cha Man City cha ligi ya mabingwa Ulaya kufikia 17 ikiwa ni mchezaji mmoja zaidi ya idadi ambayo City wanaruhusiwa kuwa nayo msimu huu baada ya kupewa adhabu kwa kuvunja taratibu za UEFA Fair Play.

City wanatakiwa kuwa na wachezaji 16 tu wa kigeni kwenye kikosi cha ligi ya mabingwa Ulaya kitakachocheza Februari 3 dhidi ya Barcelona hivyo wataweza kutatua tatizo hilo kama Jovetic atauzwa ndani ya dirisha dogo la usajili na kama itashindikana kumuuza basi kocha wa City Manuel Pellegrini atakuwa na uamuzi mgumu wa kufanya.

Wachezaji wengine ambao wana hatihati ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha Manchester City kwenye ligi ya mabingwa Ulaya ni mabeki wa pembeni Bacary Sagna na Aleksander Kolarov na kipa Willy Cabalero, wakati huo huo Pellegrini akiongelea swala hilo alisema “ lazima tutaangalia wachezaji gani hawatakuwepo kwenye kikosi cha ligi ya mabingwa kwasababu hatuna nafasi”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!