Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 January 2015
Friday, January 16, 2015

Charlie Austin mchezaji bora Desemba.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya Queens Park Rangers Charlie Austin amefanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Desemba kwenye ligi kuu nchini Uingereza huku akiwashinda Eden Hazard, John Terry, Harry Kane, Santi Carzola na David Silva.

Austin mwenye umri wa miaka 25 amenyakua tuzo hiyo baada ya kufunga jumla ya magoli matano ndani ya mwezi Desemba kati ya magoli 13 aliyonayo toka kuanza kwa msimu huu katika mashindano mbalimbali aliyocheza.

Mshambuliaji huyo wa QPR alifunga magoli hayo matano dhidi ya Burnley, Arsenal na magoli matatu (hat-trick) dhidi ya West Bromwich Albion kwenye uwanja wa Loftus Road, pia alitoa pasi moja ya goli (assist) na kupiga pasi makini 75 katika michezo sita ya Desemba ambapo alicheza kwa jumla ya dakika 435.

Baada ya kupokea tuzo hiyo akiongea na mtandao wa klabu ya QPR Austin alisema “kushinda tuzo kama hii inatia moyo, najaribu kucheza kadri ninavyoweza na kufunga magoli mengi kadri ninavyoweza kwaajili ya QPR. Lakini sio tu kuhusu mimi ni mchezo wa timu na wachezaji wenzangu wanastahili pongezi kama mimi kwa tuzo hii”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!