Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 January 2015
Saturday, January 24, 2015

Sasa Barcelona haitaki mchezo yapiga mtu goli 6-0.
Na Florence George

Klabu ya soka ya Fc Barcelona imeendelea kutoa presha kwa wapinzani wao wa karibu timu ya Real Madrid mara baada ya kushinda magoli 6-0 ya wenyeji wao timu ya Elche katika mchezo wa ligi kuu Nchini Hispania hapo jana.

Katika mchezo huo Barcelona walionekana kutawala mpira kwa kiasi kikubwa na ilifanikiwa kupata goli lake ya kwanza kupitia kwa Gerrard Pique aliyeunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Xavi Hernandez dakika ya 35.

Nyota wa timu hiyo Lionel Messi aliifungia timu yake goli la pili dakika ya 55 kwa mkwaju wa penati baada ya Neymar kuchezewa faulo ndani ya eneo la hatari.

Neymar alifunga magoli mawili ya haraka haraka katika dakika ya 69 na 71 huku pasi za magoli hayo zilizoka kwa Messi kabla ya Messi na Pedro kuhitimisha jumla ya magoli hayo.

Katika mchezo huo kocha wa Barcelona Luis Enrique alifanya mabadiliko sita katika kikosi chake ambacho kiliifunga Athletico Madrid goli 1-0 katikati ya wiki hii katika kombe la Mfalme na kumuweka benchi Luis Suarez amabaye jana ilikuwa 'birthday' yake na nafasi yake kuchukuliwa na Pedro.

Suarez ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea Liverpool na kuifungia magoli 32 msimu huu amekuwa akilalamikiwa kushuka kiwango kwani tangu ajiunge na Barcelona amefanikiwa kufunga magoli matano tu katika michezo 17 aliyocheza timu hiyo.

Sasa Barcelona wamefikisha pointi 47 katika nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya hasimu wao Real madrid yenye pointi 48 amabo wanamchezo mmoja mkononi huku Athletico Madrid wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 44 baada ya kuifunga Rayo Vallocano magoli 3-1.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!