Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 January 2015
Wednesday, January 21, 2015

Cameroon chupuchupu AFCON.


Na Chikoti Cico

Mchezo wa kundi D kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya Kameruni dhidi ya Mali uliisha kwa sare ya goli 1-1 na kufanya kila timu kwenye kundi hilo kuwa na alama moja baada ya mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Ivory Coast kuisha kwa matokeo ya sare ya goli 1-1.

Mpaka kipindi cha kwanza cha mchezo huo kinaisha hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake huku Mali wakilishambulia lango la Kameruni mara kwa mara kupitia kwa Mustapha Yatabare na Bakary Sakho.

Kipindi cha pili kilibadilika na kila timu ikionekana kutaka kupata goli huku Kameruni wakiliandama lango la Mali kupitia kwa Eric Choupo-Moting na Ambroise Oyongo lakini walikuwa ni mali waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Sambou Yatabare kwenye dakika ya 72 ya mchezo.

Goli hilo liliamsha kelele za mashabiki wa Mali kwenye uwanjwa wa Estadio de Malabo na baada ya goli hilo sehemu kubwa ya mchezo Mali walibaki kukabia chini zaidi kwenye goli lao huku wakiishambulia Kameruni kwa mipira ya kushtukiza.

Lakini walikuwa ni Kameruni waliopata goli la kusawazisha kupitia kwa Ambroise Onyongo Bitolo kwenye dakika ya 84 ya mchezo baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na Raoul Loe langoni mwa Mali.

Baada ya goli hilo Kameruni waliendelea kuliandama lango la Mali lakini mpaka mwisho wa mchezo timu hizo mbili ziligawana alama moja kwa moja, michezo inayofata kwenye kundi D itachezwa siku ya Jumamosi ambapo Mali itacheza na Ivory Coast na Kameruni kupepetana na Guinea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!