Hatimaye kocha amebadili mawazo.
Na Florence George
Baada ya kuonekana kama West Ham United msimu huu wako vizuri na wanaubavu wa kupigania moja ya nafasi nne za juu, habari mbaya kwao ni kuona kiungo wa kmataifa wa Cameroon, Alex Song akiitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon ambacho kinajiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi tarehe 17 mwezi huu huko Guinea ya Ikweta.
Alex Song ni moja ya wachezaji bora wa kocha Sam Allardyce ambaye amekuwa nguzo kwenye sehemu ya kiungo tangu alipojiunga kwa mkopo na timu hiyo ya Jijini London akitokea klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.
Pamoja na ubora wa Song bado swala ni nidhamu ni tatizo kwake hasa ukizingatia kitendo cha kipuuzi alichofanya kombe la dunia kwenye mchezo dhidi ya Croatia na kujikuta akipewa kadi nyekundu.
Tangu kumalizika kwa michuano hiyo kule nchini Brazil, Song hajawahi kuitwa kwenye timu ya taifa na hii ni mara yake ya kwanza.
Tayari West Ham United ambao wanakamata nafasi ya saba kwa sasa wakiwa na pointi 32 wamepoteza michezo migumu miwili hivi karibuni na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu kama Song, Cheikhou Kouyate na mfungaji bora wa timu hiyo, Diafra Sakho wanaojiunga na Senegal kunamuweka kocha Sam kwenye wakati mgumu.
Kocha wa timu ya taifa ya Cameroon, Volker Finke hukumjumuisha Song kwenye orodha yake ya kwanza ya wachezaji watakaoenda kwenye michuano hiyo lakini sasa amegeuza mawazo na kumjumuisha.
Wachezaji hao pamoja na mechi nyingine, watakosa mechi ngumu kama za Liverpool na Manchester United zitakazopigwa mwanzoni mwa mwezi wa pili.
0 comments:
Post a Comment