Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Gervinho nje hatua ya makundi.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa Ivory Coast na klabu ya Roma Gervinho amepewa adhabu ya kufungiwa mechi mbili baada ya kumpiga kofi kiungo wa Guinea, Naby Keita wakati wa mchezo wa kundi D kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Ivory Coast dhidi ya Guinea.

Kutokana na kitendo hicho ambacho kilipelekea Gervinho kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na kutolewa nje kwenye mchezo huo shirikisho la soka la Afrika (CAF) limeamua kumfungia mchezaji huyo kwa mechi mbili na hivyo atakosekana kwa michezo miwili ya hatua ya makundi dhidi ya Mali na Kameruni.

Pamoja na timu ya Ivory Coast kubaki na wachezaji 10 baada ya Gervinho kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo walifanikiwa kusawazisha goli la mapema la Guinea na mchezo kuisha kwa sare ya goli 1-1.

Baada ya tukio hilo Gervinho aliomba msamaha kwa nchi yake, wachezaji wenzake, mashabiki na waandaaji wa michuano hiyo kwa kitendo chake hicho cha hasira kupitia kwenye ukurasa wake tweeter.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!