Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 January 2015
Thursday, January 22, 2015

Simeone aikataa Real Madrid na Brazili.Na Chikoti Cico

Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone ameapa kamwe hatazifundisha timu za Real Madrid ambao ni wapinzani wakubwa wa Atletico Madird nchini Hispania na timu ya taifa ya Brazili maarufu kama “Sellecao” ambao ni wapinzani wakubwa wa Argentina, taifa ambalo ndipo anatokea kocha huyo. 

Kocha huyo ambaye aliiongoza klabu ya Atletico Madrid kunyakua kombe la ligi kuu nchini Hispania kwenye msimu wa mwaka 2014/2015 huku ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 1996 walipoweza kunyakua kombe hilo kwa mara ya mwisho na kuifikisha fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya amekuwa akihusishwa kuhamia klabu mbalimbali. 

Lakini kocha huyo akiongelea kuhusu kuzifundisha Real Madrid na Brazili wakati akiongea na mtandao wa FIFA alisema “nitazifundisha Real Madrid na Brazili kama nikipewa mkataba mzuri usiofikirika na pesa bila kikomo? Nadhani nitauacha na kusema kwaheri kwa pesa” 

Pia kocha huyo aliongelea uwezekano wa kuifundisha timu ya taifa ya Argentina na kusema “sikupewa kazi ya Argentina baada ya kombe la Dunia lakini najua itatokea siku moja”. 

Aliendelea kusema “mara kwa mara nimesema kwa timu ya taifa kuna nafasi kwa kile ninachokiita mtoto, baba na babu aina ya kufundisha, nadhani ni sehemu kwaajili ya babu mtu mtulivu zaidi na makini ambaye anaona mambo kwa njia tofauti” “Bado nahisi nahitaji kuwepo uwanjani, kufanya mafunzo na kuwa na wachezaji kila siku, timu ya taifa haiwezi kukupa hayo. 

Ni kitu ambacho ningependa kufanya siku moja? Hakika! Nilitumia miaka 12 ama14 na timu ya taifa ulikuwa muda wa faida na sehemu kubwa ya maisha yangu, natumai itakuja kupita kwa muda muafaka kwa pande zote mbili”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!