Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 January 2015
Thursday, January 15, 2015

Leighton Baines ni beki bingwa wa “assist”


Na Chikoti Cico

Wakati beki na nahodha wa klabu ya Chelsea, John Tery akikaribia kuvunja rekodi ya beki mwenye magoli mengi kwenye historia ya ligi kuu nchini Uingereza, huku rekodi hiyo ikiwa ni magoli 38 iliyowekwa na David Unsworth na mpaka sasa Terry akiwa ameshafunga magoli 37, Leighton Baines anaongoza kwa pasi za magoli yaani “assist”.

Beki huyo wa kushoto wa timu ya Everton anaongoza kwenye orodha ya mabeki wenye pasi nyingi za magoli kwenye historia ya ligi kuu nchini Uingereza huku mpaka sasa akiwa amepiga pasi 45 katika michezo mbalimbali ya ligi hiyo.

Anayemfwatia kwa karibu Baines ni beki wa zamani wa Uingereza Graeme Le Saux ambaye aliwahi kuzichezea klabu za Chelsea, Blackburn Rovers na Southampton ambaye ana “assist” 44.

 Ian Harte anbaye aliwahi kuzichezea klabu za Leeds United na Sunderland na beki wa zamni wa Manchester City na Everton, Andy Hinchcliffe wote wawili wanashika nafasi ya tatu wakiwa na “assist 36 kila mmoja huku beki wa kulia wa zamani wa Manchester United Gary Neville akishika nafasi ya nne akiwa na “assist” 35.

Baines anaonekana ataendelea kuongoza kwenye orodha hiyo ya mabeki wenye “assist” nyingi kwani mabeki wote wanaomfwatia kwa karibu wameshastaafu kucheza soka katika ngazi ya ligi kuu nchini Uingereza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!