Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 December 2014
Friday, December 05, 2014

Yanga vs Express kesho Uwanja wa Taifa.



Klabu ya soka ya Yanga, ya Jijini Dar es Salaam kesho itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Soka ya The Express Kutoka nchini Uganda, mchezo utakaochezwa majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika dimba la Uwanja Taifa Jijini Dar es salaam.
 
Yanga itapambana na The Express kama sehemu ya mchezo wa maandalizi ya kujipima nguvu kuelekea pambano la mtani jembe siku ya jumamosi tarehe 13/12/20014 dhidi ya timu ya Simba SC jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kesho kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo anatarajiwa kukitumia kikosi chake chote kwa lengo la kutazama maendeleo ya vijana wake kabla ya mchezo wa Nani Mtani Jembe wiki ijayo.

Mpaka sasa klabu ya Young Africans imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu Emerson De Oliveira kutoka nchini Brazil ambaye anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santana "Jaja" ambaye ameomba kuachwa kutokana na kushindwa kurejea nchini kwa masuala ya kifamilia. 

Wananchama, mashabiki na wapenzi wa Yanga kutoka matawi mbalimbali wanaombwa kuhudhuriwa kwa wingi uwanjani, ili kutoa hamasa ya ushindi kwa wachezaji siku ya jumamosi katika uwanja mkuu wa taifa, jijini Dar es salaam.

Yanga inashiriki ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa inashika nafasi ya pili sawa na Azam FC kwa kulingana pointi na magoli ya kufunga na kufunga, inajaindaa pia na mzunguko wa nane wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa kombe la Shirkisho baranai Afrika mapema mwakani.

Source: website ya Yanga.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!