Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

Alexies Sanchez kupewa likizo ya wiki moja.



Na Florence George

Mshambuliaji wa Arsenal, Alexies Sanchez anaonekana kumpagawisha kocha wa timu hiyo Mfaransa, Arsene Wenger kutokana na kiwango bora kilichoonyeshwa na mchezaji huyo tangu alipojiunga na washika bunduki hao wa London msimu huu akitokea klabu ya Barcelona.

Wenger ameweka wazi kuwa, kilichomfanya nyota huyo ambaye ni raia wa Chile kushindwa kutamba akiwa na Barcelona, ni mfumo wa klabu hiyo ambao umejengwa kwa kumzunguka mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi. 

Wenger amewataja pia wachezaji bora kama David Villa, Thierry Henry, Zlatan Ibrahimovic kuwa nao walishindwa kutamba na Wakatalunia hao kwa sababu ile ile ya uwepo wa Messi.

Wenger ameendelea kusema kuwa, Sanchez kwa sasa anaonekana kucheza vizuri ni kwa sababu anapata mipira mara nyingi na yuko huru kutamba kila kona ya uwanja kitu ambacho alikuwa hakipati akiwa na Barcelona.

Sanchez tayari amefunga magoli 14 kwenye mechi 18 ambazo ameitumikia klabu ya Arsenal. Kocha huyo amepanga kumpatia Sanchez wiki moja ya mapumziko mara baada ya mchezo wao wa leo dhidi ya Stoke City.

Ukijumuisha mechi za kimataifa, Sanchez tayari amecheza michezo 27 na Wenger amepanga kumpuzisha ili kupata kilicho bora kutoka kwake. Alikuwa anafanya hivyo kwa Thierry Henry, Roben Van Persie na sasa ni zamu ya Alexies.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!