Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 December 2014
Wednesday, December 31, 2014

Uchambuzi: Stoke City vs Manchester United


Na Chikoti Cico

Mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Uingereza unatarajiwa kuanza siku ya Ijumaa ikiwa ni tarehe mosi ya mwezi wa kwanza kwa mwaka 2015, na mechi ya kwanza kabisa itapigwa kwenye uwanja Britannia kati ya Stoke City dhidi ya Manchester United majira ya saa 9:45 Alasiri.

Stoke City ambao wanashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 25 wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kwa nguvu kutafuta alama tatu muhimu na kuweza kuanza vyema mwaka mpya wa 2015.

Kocha wa Stoke, Mark Hughes kuelekea mchezo huo atamkosa mshambuliaji wake Bojan Krkic aliyeumia kwenye mchezo dhidi ya Everton siku ya “boxing day” pia atawakosa Phil Bardsley, Stephen Ireland,Victor Moses na Pete Odemwingie ambao nao ni majeruhi.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Stoke wamekuwa na rekodi mbaya dhidi ya United kwani katika michezo 13 iliyopita ya ligi wameshinda mchezo mmoja tu huku wakifungwa michezo 11 na kutoka sare mchezo mmoja.

kikosi cha Stoke kinaweza kuwa hivi: Begovic; Cameron, Shawcross, Muniesa, Pieters; N'Zonzi, Whelan; Arnautovic, Adam, Walters; Diouf

Kwa upande wa Manchester United kiungo wa timu hiyo Angel di Maria ambaye alikuwa majeruhi na kukosekana kwa mechi zilizopita amerejea mazoezini na anaweza kucheza mchezo huo.

Pia Adnan Januzaj na Ander Herrera ambao nao walikuwa majeruhi walifanya mazoezi wiki hii hivyo wanaweza kucheza dhidi ya Stoke lakini Marcos Rojo, Daley Blind na Marouane Fellaini wataendelea kukosekana kwenye mchezo huo.

Manchester United inayofundishwa na kocha Louis van Gaal mpaka sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 36 hivyo inatarajiwa kupigana kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kuzifukuzia kileleni timu za Manchester City na Chelsea.

Takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa Manchester United, Robin va Persie ana rekodi nzuri ya magoli dhidi ya Stoke kwani katika michezo 10 aliyocheza dhid yao amefunga goli 10 huku magoli manne kati ya hayo akiyafunga katika mechi tano alizocheza akiwa na Manchester United.

Kikosi cha Manchester United kinaweza kuwa hivi: De Gea; Jones, Smalling, Evans; Rafael, Carrick, Rooney, Shaw; Mata; Van Persie, Wilson

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!