Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 December 2014
Wednesday, December 31, 2014

Uchambuzi: Liverpool vs Leicester City


Na Chikoti Cico

Kwenye uwanja wa Anfield wenyeji timu ya Liverpool wanatarajiwa kuikaribisha timu ya Leicester City katika moja ya michezo ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Uingereza.

Liverpool wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Swansea siku ya Jumatatu iliyopita na kupelekea kushika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 28 hivyo wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na ari ya kutafuta alama nyingine tatu muhimu.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers kuelekea mchezo huo atamkosa beki wake mahiri Martin Skrtel ambaye amesimamishwa baada ya kupata kadi ya tano ya njano kwenye mchezo uliopita dhidi ya Swansea,

Pia atamkosa beki wa katikati Dejan Lovren ambaye alikuwa na majeraha ya mtoki na ambaye alikosekana kwenye mechi tatu zilizopita, ingawa amerejea mazoezini lakini atakosekana dhidi ya Leicester hivyo anatarajiwa kurejea kwenye mchezo wa kombe la FA.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Liverpool wana rekodi nzuri na mechi zinazochezwa siku ya mwaka mpya kwenye uwanja wao wa Anfield kwani katika michezo saba waliyocheza, wameshinda michezo mitano huku wakifungwa mchezo mmoja tu na kutoka sare mchezo mmoja.

Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Can, Toure, Sakho; Henderson, Gerrard, Lucas, Coutinho, Moreno; Lallana, Sterling

Leicester City wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kupigana kufa na kupona kupata alama tatu kwani mpaka sasa wanashika mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 13 huku wakiwa na hatari ya kushuka daraja.

Kocha wa Leicester, Nigel Pearson atamkosa beki wake wa kulia Paul Konchesky ambaye amesimamishwa baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Hull City pia atawakosa Andy King, Kasper Schmeichel na Matt Upson ambao ni majeruhi huku Jamie Vardy akitarajiwa kurejea kikosini baada ya kusimamishwa.

Takwimu kuelekea mchezo huo zinaonyesha wachezaji wa tatu wa Leicester Taylor-Fletcher, Nugent, Konchesky ambao wameshawahi kufunga magoli dhidi ya Liverpool hakuna ambaye amewahi kufunga goli kwenye uwanja wa Anfield.

Kikos cha Leicester City kinaweza kuwa hivi: Hamer; Simpson, Morgan, Wasilewski, De Laet; Mahrez, James, Cambiasso, Schlupp; Nugent, Ulloa

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!