Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 December 2014
Tuesday, December 16, 2014

Mourinho hana masihara msimu huu.Na Oscar Oscar Jr

Magoli kutoka kwa Eden Hazard 23, Filipe Luis 56 na Andre Schurrle 82 yalitosha kuwafikisha hatua ya nusu fainali vijana wa Chelsea kwenye kombe la ligi dhidi ya Derby Country mchezo ulioshuhudia beki wa kimataifa wa Ufaransa, Kurt Zouma akiumia na kutolewa nje.

Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa bao 3-1 mbele ya Derby ambao walikuwa wamepania kupata ushindi hapo jana. 

Mourinho kuonyesha kuwa alikuwa amepania mchezo huo, alifanya mabadiliko matano tu kwenye kikosi ambacho kilicheza na Hull City wiki iliyopita.

Didier Drogba, Azpilicueta, Zouma, Schürrle na Fàbregas waliingia baadaye kwenye kikosi hicho ambacho kilikuwa tayari na watu kama Nahodha, John Terry, Cech, Mikel John Obi, Eden Hazard, Filipe Luís na Nemanja Matic.Mourinho amezungumza kuwa bila kufanya hivyo, wngeweza kupoteza mchezo wa jana.

Mourinho ambaye msimu uliopita alitoka bila taji lolote akiwa na Chelsea, amejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa taji hilo ambalo wakati anakuja kuinoa Chelsea kipindi cha kwanza akitokeo Ureno, ndilo lililokuwa pia taji lake la kwanza kwenye safari yake ya mafanikio.

Akizungumzia kuumia kwa Kurts Zouma, Mourinho amesema sio tatizo kubwa sana na mchezaji huyo huenda akacheza kwenye mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Stoke City siku ya Jumatatu. 

Chelsea bado wanashiriki kwenye mashindano yote manne msimu huu huku wakionyesha kujipanga kwa kila shindano.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!