Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 December 2014
Tuesday, December 16, 2014

Tuzo zamwagika kwa Wadachi wa Manchester United. Na Oscar Oscar Jr

Kocha wa kimtaifa wa Uholanzi na klabu ya Manchester United, Loius Van Gaal usiku wa Jumanne ya jana aliweza kutangazwa kama kocha bora wa mwaka nchini Uholanzi baaada ya kuiwezesha nchi hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia kule nchini Brazil.

Van Gaal ambaye kwa sasa ni kocha wa Manchester United, aliweza kutwaa zawadi hiyo huku Roben Van Persie ambaye pia ni mchezaji wa Manchester United akifanikiwa kupata tuzo ya goli bora la mwaka. 

Goli ambalo limemfanya Van Persie aweze kupewa tuzo hiyo ni lile alilofunga kwa kichwa kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa Hispania.

Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, Ajen Roben ametangazwa kama mchezaji bora wa mwaka 2014 wa Uholanzi baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa na klabu ya Bayern Munich na kuwa sehemu ya timu ya taifa ya Uholanzi ambayo ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye michuano ya kombe la dnnia.

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Arjen Roben alishindwa kuhudhuria sherehe hizo kutokana na kuwa na majukumu na klabu yake ya Bayern Munich na hivyo hotuba yake ilitazamwa kupitia Luninga.

kikosi cha kocha Pep Guardiola kilikuwa na mechi ya Bundesliga ambayo iliwakutanisha na timu ya Freiburg na vijana wa Bayern Munich walifanikiwa kushinda mabao 2-0 huku Roben akiwa moja ya wafungaji kwenye ushindi huo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!