Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 December 2014
Tuesday, December 16, 2014

Barcelona yampiga mtu goli 12Barcelona imeamua kumwaga njumu kwa watoto wa ligi daraja la tatu, timu ya Huesca kwenye mchezo wa kombe la Mfalme. Mchezo wa kwanza ugenini ulishuhudia Barcelona wakipata ushindi wa ba 4-0 huku mchezo wa marudiano ukishuhudia Barcelona wakipata ushindi wa mabao 8-1.

Barcelona katika mchezo huo wa marudiano, ilishuhudia Luiz Suarez, Neymar Jr na Lionel Messi wakipumzishwa lakini Huesca hawakuweza kufurukuta na kujikuta wakichezea kipigo cha mbwa mwizi. 

Pedro Rodriquez alifunga Hat Trick ndani ya dakika 45 za kwanza huku Anders Iniesta na Sergi Roberto nao wakifunga kabla ya mapumziko.

Matokeo hayo yanawafanya Barcelona wafuzu kwa uwiano wa mabao 12-1 na hatua inayofuata ya 16 bora ya michuano hiyo wanaweza kukutana na ama Elche au Valladolid.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!