Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Timua timua ya makocha yaanza EPL



Na Chikoti Cico
 
Kocha wa Crystal Palace, Neil Warnock afukuzwa kazi na timu hiyo baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza huku mpaka sasa ikishika nafasi ya 18 ikiwa na alama 15 huku wakiwa na hatari ya kushuka daraja.

Warnock ameiongoza timu hiyo kwa miezi minne tu katika mechi 16 za ligi kuu nchini Uingereza toka aliposaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo tarehe 28 mwezo wa nane akichukua nafasi ya Tony Pulis.

Mtandao wa Crystal Palace ulithibitisha kufukuzwa kwa Warnock ukiandika “klabu ya Crystal Palace inathibitisha leo kwamba Neil Warnock ameachishwa majukumu yake na sio tena Meneja wa timu, klabu ingependa kuweka kwenye rekodi shukrani zake kwa Neil kwa juhudi na nguvu zake kwa miezi minne iliyopita”.

“Keith Millen ataiongoza timu dhidi ya Queens Park Rangers kesho (Jumapili) kama Meneja wa muda”

Mwenyekiti wa Crystal Palace, Steve Parish akielezea sababu ya kumfukuza kocha huyo na taratibu za kutafuta Meneja mpya alisema “ Tumemwacha Neil aende na tumemshukuru kwa kazi yake, mmiliki wa Palace amesema “mambo hayaendi sawa na tunaangalia majibu dhidi ya QPR”

Aliendelea kusema “Nililalia hakika kwenye hili na kuongea na watu wachache na nikafanya uamuzi asubuhi hii. Neil ni mtu mzuri na alitaka kufanya hapa Palace haikutokea, haifanyi kazi, wakati wote unataka mambo yawekwe sawa mapema iwezekanavyo lakini sijapata mtu yeyote, tunataka kufanya mazungumzo mapema iwezekanavyo”.

Mpaka sasa makocha ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Neil Warnock ni kocha wa zamani wa Spurs Tim Sherwood, Chris Hughton na kocha wa zamani wa timu hiyo Tony Pulis.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!