Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

Carlo Ancelotti kuongezewa mwaka mmoja


Na Chikoti Cico

Kocha wa Real Madrid kutoka nchini Italia, Carlo Ancelotti anatarajia kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo kutoka nchini Hispania. Taarifa kutoka gazeti la Marca la nchini humo zinasema Ancelotti amekubali kutia saini kuendelea kujikita zaidi na mabingwa hao watetezi wa Ulaya.

Ancelotti ambaye ameiongoza Madrid kuchukua kombe ligi ya mabingwa Ulaya kwenye msimu uliopita kwa kuifunga timu ya Atletico Madrid, Amekuwa na mwanzo mzuri kwenye ligi kuu nchini Hispania maarufu kama la liga huku mpaka sasa Madrid ikiwa inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 33.

Akiwa ameshawahi kuzifundisha timu za AC Milan, Juventus, Chelsea na PSG na kuziwezesha timu hizo kunyakua makombe mbalimbali, kocha huyo ameendelea kuonyesha umahiri wake akiwa na Madrid mpaka kufikia hatua ya kutaka kuongezewa mkataba mpya.

Mkataba wa sasa wa kocha huyo aliyejiunga na Madrid mwezi Juni 2013 akitokea timu ya PSG, utaisha mwakani 2016 hivyo taarifa za kukubali kuongezewa mwaka mmoja zitawapa furaha mashabiki wa timu hivyo maarufu kama “los blancos”

Wakati huo huo taarifa nchini Hispania zinasema timu ya Real Madrid ambayo inafukuzia rekodi ya kushinda mechi 18 mfululizo, inakaribia kumsajili kiungo kutoka klabu ya Cruzeiro ya nchini Brazili, Lucas Silva mwenye umri wa miaka 21.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!