Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

arsenal yalambishwa mchanga na stoke city



Na florence george

Mara baada ya kupata ushindi dhidi ya southampton katikati ya wiki hii timu ta soka ya arsenal leo imekumbana na kipigo kutoka kwa timu ya stoke city cha magoli matatu kwa mawili katika dimba la  britannia stadium

 kabla ya mchezo huo timu ya arsenal ilikuwa katika nafasi ya sita huku ikiwa na pointi 23 huku timu ya stoke city ilikuwa anafasi ya kumi na mbili  huku ikiwa na pointi 15.

katika mchezo huo ulishuhudia timu ya stoke city ikitawala kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata magoli kupitia kwa peter crouch,walters samwel pamoja na bojan krkric katika kipindi cha kwanza kabla ya arsenal kuzinduka kipindi cha pili na kufanikiwa kupata angalau magoli mawili yaliyofungwa na santi cazorla na Aaron ramsey.

pia katika dakika ya 78 ilishudiwa mchezaji wa arsenal calum chambers akionyeshwa kadi ya pili ya njano hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu hali iliyopunguza kasi kwa vijana hao wa london katika juhudi za kusawazisha goli la tatu.

kwa matokeo hayo yanawaweka pabaya vijana wa arsenal katika haraki za kuingia nafasi za nne za juu kwani hadi sasa inazidiwa pointi 2 na manchester united iliyopo nafasi ya nne huku ikiwa na mchezo mmja mkononi,huku ikizidiwa pointi 13 na vinara wa ligi hiyo timu ya chelsea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!