Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 January 2015
Sunday, January 11, 2015

Pep Gaurdiola aitolea nje Barcelona.
Na Oscar Oscar Jr

Bado mambo sio shwari kwenye klabu ya Barcelona na sasa kumekuwa na habari za timu hiyo kutaka kumrejesha kocha wa sasa wa Bayern Munich, Pep Gaurdiola. 

Bareclona wako mbioni kumtimua kazi kocha wa sasa Luiz Enrique kufuatia kocha huyo kutoelewana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.

Kocha Pep Gaurdiola ambaye aliwahi kuifundisha timu hiyo na kutwaa kila kikombe kinachopiganiwa kwa ngazi ya vilabu, ameibuka na kusema kuwa hana mpango wa kurudi tena Barcelona na hali ya sintofahamu iliyoendelea ndani ya klabu hiyo haiwezi kutatuliwa kwa yeye kurejea.

Barcelona wamekuwa na matukio matatu ambayo yanaonekana kuwatikisa kwa siku za hivi karibuni moja ikiwa ni kufungiwa kufanya usajili kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia katika kesi yao ya kusajili wachezaji vijana wa kigeni kinyume na taratibu.

Mambo mengine yanayoikumba Barcelona ni kumtimua kazi mkurugeni wa ufundi wa timu hiyo na mwisho ni swala la kocha Enrique kutoelewana na baadhi ya mastaa akiwemo, Lionel Messi.

Katika habari zilizotoka leo zinadai kuwa, bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo baada ya kushindwa kumrejesha Pep Gaurdiola, wamejiandaa kumuomba aliyekuwa kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes arejea kutoka kustaafu na kuja kuokoa jahazi lao ambao wanadhani linaelekea kuzama.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!