Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 November 2014
Friday, November 07, 2014

Uchambuzi: Liverpool vs Chelsea


Na Chikoti Cico

Ligi kuu nchini Uingereza inatarajiwa kuendelea tena leo huku moja ya mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu ikiwa ni kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Anfield.

Ni mechi kama hii kwenye msimu uliopita iliwakosesha Liverpool ubingwa baada ya Chelsea kushinda kwa magoli 2-0.
Baada ya kuwapumzisha wachezaji saba wa kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kwaajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Chelsea.

Kitendo hicho kilileta hali ya sintofahamu kwa kocha wa Liverpool Brendan Rodgers kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa soka na mashabiki wa Liverpool kinaonekana kuongeza presha ya kushinda mchezo dhidi ya Chelsea kwa kocha huyo.

Liverpool inayoshika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 14 itaendelea kuwakosa Daniel Sturridge, Jon Flanagan, Suso, Jose Enrique na Mamadou Sakho ambao ni majeruhi huku kocha Brendan akitarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta ushindi wake wa kwanza dhidi ya bosi wake wa zamani.

Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno; Henderson, Gerrard, Allen, Coutinho; Sterling, Balotelli

Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 26 wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutaka kuendeleza rekodi ya kutokufungwa toka kuanza kwa msimu wa 2014/15.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anataendela kumkosa mshambuliaji Loic Remy ambaye ni majeruhi hivyo safu ya ushambuliaji ya Chelsea inatarajiwa kuongoza na Diego Costa ambaye alikosekana kwa zaidi ya mechi tatu zilizopita za ligi.

Mpaka sasa Costa ana magoli tisa kati ya mechi nane alizocheza.
Takwimu zinaonyesha kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amecheza mechi 18 dhidi ya Liverpool na kusinda michezo tisa, kutoka sare michezo minne na kufungwa michezo mitano, huku akiwa amecheza michezo mitano Anfield na kushinda michezo mitatu, kutoka sare mchezo mmoja na kufungwa mchezo mmoja.

Kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: ourtois; Ivanovic, Terry, Cahill, Azpilicueta; Matic, Fabregas, Ramires; Oscar, Hazard; Costa

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!