Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 November 2014
Thursday, November 27, 2014

Real Madrid 1-0 Basel, Ronaldo amkaribia Lionel Messi.


Baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Basel, klabu ya Real Madrid imejihakikishia nafasi ya kuwa vinara wa kundi B baada ya kushinda michezo yake yote. 

Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa Ulaya, walimkosa kwenye mchezo huo, Kiungo Luke Modric ambaye ni majeruhi huku Pepe na Khedira wakipumzishwa.

James Rodriguez na Gareth Bale walikuwa mwiba mchungu kwa timu ya Basel lakini, hawakufanikiwa kupata bao licha ya kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo. 

Goli la Christiano Ronaldo, linamfanya awe sawa na Gwiji wa zamani wa Real Madrid, Raul Gonzalez ambaye alifunga mabao 71. Ronaldo amefikisha mabao hayo na sasa, ni mapambano dhidi ya mpinzani wake Lionel Messi ambaye amefikisha rekodi ya mabao 74.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!