Pep Gaurdiola kuinoa klabu ya Arsenal
Na Oscar Oscar Jr
Karibu wiki nzima kumekuwa na taarifa za klabu ya Arsenal kutafuta kocha wa kurithi mikoba ya kocha wa sasa wa klabu hiyo, Mfaransa Arsene Wenger.
Siku mbili za hivi karibuni, majina ya kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti na baadaye msaidizi wake, Paul Clement yalitajwa miongoni mwa watu wakuchukuwa nafasi ya Wenger.
Jana kulikuwa na habari za kocha wa Burussia Dortimund, Jurgen Klopp naye kutajwa kwenye dili la kutua kwa washika Bunduki hao lakini, Gazeti la The Evining Standard leo hii limetoa taarifa kuwa, kocha Pep Gaurdiola wa klabu ya Bayern Munich ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuichukuwa nafasi ya Wenger.
Pep Gaurdiola inasemekana ni muumini mkubwa wa timu ya Arsenal na amekuwa akipigiwa upatu kwa sababu, aina ya ufundishaji wake unashabihiana na namna utamaduni wa soka la Arsenal ulivyo.
Pep anadaiwa kuwa tayari kuchukuwa nafasi hiyo mwaka 2016 pale mkataba wake wa sasa na Bayern Munich utakapokuwa umemalizika.
Bado hakuna chombo chochote cha habari kinachoelezea sababu za kocha Arsene Wenger, kutaka kuacha kuinoa timu hiyo ambayo alianza kuiongoza tangu mwaka 1999.
Baada ya kocha huyo kuacha kazi ya kuifundisha timu hiyo, inaelezwa kuwa, ataenda kuungana na kuwa sehemu ya wakurugenzi wa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment