Mourinho asema "Bado nipo nipo sana"
Na Oscar Oscar Jr
Vinara wa ligi kuu ya Uingereza, timu ya Chelsea leo hii itashuka Darajani kupambana na timu ya QPR na tayari makocha wa timu hizo wameanza kurushiana maneno.
Kocha wa QPR, Harry Redknapp amesema kuwa, Jose Mourinho amefanikiwa katika kazi yake kutokana na kufanya kazi kwenye klabu ambazo zipo vizuri kiuchumi.
Mourinho kwa upande wake, amejibu hilo kwa kusema kuwa ni kweli amefanya kazi na kwabu kubwa lakini hazikuwa klabu bora. Mourinho ametolea mfano klabu za Porto, Chelsea na Inter Millan kuwa pamoja na kuwa zilikuwa klabu kubwa lakini hazikuwa klabu bora duniani.
Kocha huyo wa Kireno aliendelea kusema kuwa, kila timu inachangamoto zake. Kufanya kazi kwenye timu bora ni vigumu kwa sababu matarajio ni makubwa sana.
Mourinho hakusita kusema pia, hata kufundisha timu ndogo nako kunachangamoto zake kwani unatakiwa kuhakikisha timu haishuki daraja.
Kwa upande mwingine, Mourinho aliulizwa kama anatarajia kustaafu kufanya kazi ya ukocha hivi karibu, alijibu kuwa, hafikirii hilo kwa sasa.
Anampango wa kuifanya kazi hiyo kwa miaka 15 hadi 20 ijayo. Mourinho ana miaka 51 kwa sasa na amepanga kuwa kocha hadi atakapofikia miaka 70.
0 comments:
Post a Comment