Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 November 2014
Saturday, November 01, 2014

Thibaut Courtois aipa ubingwa wa EPL na UEFA timu ya Chelsea


Na Rossa Kabwine

Golikipa wa timu ya Chelsea, Thibaut Courtois anasema Chelsea inaweza kuchukua ubingwa wa Uingereza na wa klabu bingwa Ulaya msimu huu. 

Chelsea ambayo inaongoza ligi kuu ya Uingereza ikiwa mbele kwa pointi nne zaidi ya Southampton inayoshika nafasi ya pili,  wanaongoza pia  kundi lao la Uefa baada yakucheza michezo mitatu na kuvuna pointi saba.

Courtois ambaye amekuwa kipa chaguo la kwanza mbele ya Peter Cech, amezungumza kuwa, Chelsea ina kikosi bora ambacho kinaweza kuchukua taji la ligi kuu Uingereza na lile la Mabingwa Ulaya ambalo linashikiliwa na klabua ya Real Madrid.

Kipa huyo kutoaka Ubelgiji alieleza kuwa, timu ya Chelsea iko vizuri kuanzia wachezaji 11 wanaoanza kwenye kikosi cha kwanza mpaka wale wanaotokea benchi.

Pamoja na kusifia kikosi chake, kipa huyo hakusita kutaja timu nyingine ambazo anadhani kuwa ni bora na zinaweza kutwaa taji hilo la Ulaya msimu huu.

Courtois alizitaja timu za Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich kuwa washindani wao wakubwa msimu huu kwenye klabu bingwa Ulaya na kukiri kuwa, Chelsea inahitaji kuwa na bahati pia katika hilo.

Courtois alijiunga na klabu ya Chelsea akitokea Genk mwaka 2011 lakini alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania kwa muda wa miaka mitatu.

Courtois ameshinda kombe la La Liga msimu uliopita na kucheza fainali ya Uefa akiwa na klabu ya Atletico Madrid na kupoteza mchezo huo kwa mahasimu wao, timu ya Real Madrid.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!