Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 November 2014
Tuesday, November 04, 2014

Mshambuliaji Ame Ally kutua Msimbazi


Na Oscar Oscar Jr

Mshambuliaji wa klabu ya Mtibwa Sugar, Ame Ally ni moja kati ya majina yanayozungumzwa sana msimu huu kwenye ligi kuu Tanzania bara kutokana na umahiri aliyoonyesha mpaka sasa. Ame ambaye alisajiliwa akitokea klabu ya Chuoni inayoshiriki ligi kuu Zanzibar, amefunga magoli matatu kwenye mechi sita alizocheza mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwanaspoti la leo, mshambuliaji huyo amehusishwa na kujiunga na klabu ya Simba kwenye dirija dogo la usajili ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi Novemba 15 na kufungwa Desemba 15.

Ame amewekwa kwenye mipango ya klabu ya Simba na kiasi cha pesa kilichotajwa kumunasa mshambuliaji huyo ni Milion 40. Mtibwa Sugar ni klabu inayofanya vizuri kwasasa huku ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kujikusanyia pointi 14.

Timu ya Coastal Union ya Tanga, inashikilia nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama 11 huku Azam wakisalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa sawa na Yanga walioko kwenye nafasi ya nne wote wakiwa na alama 10. Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena weekend hi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!