Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 November 2014
Thursday, November 27, 2014

Messi hafikii hata nusu ya Uwezo wa Ronaldo.


Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela ameibuka na kudai kuwa, mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hafiki hata nusu ya ubora wa Cristiano Ronaldo. Carlos Vela aliyasema hayo wakati akizungumza na kituo kimoja cha Redio nchini Hispania.

Vela amesema kuwa, watu wengi wanamuonea wivu Christiano Ronaldo na ndiyo maana unaweza kumuona akishinda Ballon D'or mara mbili tu. 

Vela amesema, muonekano wa Ronaldo na utanashati wake ni moja kati ya sababu zilizofanya achukiwe na watu wengi na kukosa kutangazwa mchezaji bora wa Dunia mara nyingi kuliko Lionel Messi.

Lionel Messi hivi karibuni amevunja na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu nchini Hispania na kuweka rekodi mpya kama mfungaji bora wa muda wote wa michuano ya klabu bingwa Ulaya. 

Vela bado umeshindwa kumsifia Messi huku akisema kuwa, ukitazama muda wa Ronaldo kucheza La Liga na magoli aliyofunga, haina ubishi kuwa Messi hafiki hata nusu ya Ronaldo. Vela pia amesema, Ronaldo ameonyesha uwezo kwenye ligi nyingi kuliko Messi ambaye ameganda kwenye ligi moja tu.

 Ronaldo tayari amefunga magoli 277 kutokana na kucheza mechi 264 tangu aliondoka Manchester United na kutua Loc Blancos mwaka 2009, mara kadhaa amekuwa akilinganisha na Messi  ambaye amefunga magoli 371 katika mechi 442 akiwa na Barcelona.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!