Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 November 2014
Tuesday, November 11, 2014

Ibrahimovic anyakua tuzo nchini Sweden.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden na timu ya Paris Saint Germain (PSG) ya nchini Ufaransa amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka nchini Sweden kwa mara ya tisa mfululizo tokea kuanzishwa kwa tuzo hiyo miaka 10 iliyopita, tuzo hiyo imepewa jina la Guldbollen (mpira wa dhahabu).

Mshambuliaji huyo ambaye amewahi kukipiga timu za Ajax, Juventus, Inter Milan na Barcelona pia anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa timu ya taifa ya Sweden akiwa amefunga magoli 50 kati ya michezo 99 alizoichezea timu hiyo.

Tukio la utoaji wa tuzo pia lilienda sambamba na kumbukumbu ya wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Sweden waliofariki ambao ni kiungo Klas Ingesson ambaye alifariki kwa ugonjwa wa kansa na beki Pontus Segerström ambaye alifariki kwa kuwa na uvimbe kwenye ubongo.

Baada ya kupewa tuzo hiyo Ibrahimovic aliongelea vifo vya wachezaji hao wawili wa zamani wa Sweden kwa kusema “ tuzo hizi zote nilizopokea zinamaanisha kwamba nimefanikiwa kitu, na kwamba niko vizuri kwa kile ninachokifanya lakini zimefunikwa na kivuli kwa kilichotokea kwa Klas Ingesson na Pontus Segerstrom”

Sambamba na kuongelea vifo vya wachezaji hao wa timu ya taifa ya Sweden pia Ibrahimovic alizungumzia kifo cha kaka yake Sapko aliyefariki mwezi Aprili kwa kusema ”Nilikuwa na kaka aliyefariki miezi michache iliyopita kwa ugonjwa kama huo (Kansa). Kuna maisha zaidi ya soka na hilo ni muhimu zaidi kuliko hili (kushinda tuzo) hivyo…. wapumzike kwa amani.

Toka kuanzishwa kwa tuzo hiyo ni mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Freddie Ljundberg peke ndiyo amewahi kunyakuwa zaidi ya Ibrahimovic

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!