Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 August 2014
Monday, August 04, 2014

MACHOZI YA KINAFIKI YA SHOMARI KAPOMBE


Na mwandishi wetu.

Naamka jumatatu asubuhi nikiwa tayari kwa mapambano ya nchi na kutafuta chochote kitu ili watoto waweze kupata ugali. kama kawaida kwa ilivyo vijana wa kitanzania wa sasa nakamata smartphone yangu nakuingia kwenye mitandao ya kijamii kuperuzi na kupata habari mbalimbali. Mara nakutana na habari pamoja na picha za mechi  kati ya Taifa Stars na Msumbiji iliyochezwa jana mjini Maputo.

Hapa nakutana na picha za kusikitisha sana za wachezaji wetu wengi wakiwa na huzuni, na kwa masikitiko makubwa wanahuzunika kwa matokeo waliyoyapata.

Nasikitika sana haswa kuona kijana mwenzangu wa kitanzania akilia kwa uchungu lakini kwa upande mwingine nacheka sana maana nilijua kilichotupeleka Maputo Msumbiji ni kwenda kukamilisha ratiba tu maana mchezo ulikuwa umeisha tangu Uwanja wa Taifa Dar es saalam.

Ushindi wa ugenini ilikuwa kazi ngumu sana kwetu haswa ukizingatia tuliwapa Mambaz nafasi ya kutikisa wavu wetu pindi walipokuja kwetu.

Magoli mawili ya Khamis Mcha “Viali” kwenye mechi ya nyumbani hayakuwa na thamani mbele ya mambaz wenye kiu ya chakula, na hata goli moja la Mbwana Samata “SAMAGOAL”  halikuwa na nafasi ya kulisukuma gurudumu letu mbele ya safari.

Nazidi kucheka kwa kujifariji maana hili suala sio mara ya kwanza kututokea kamailivyo kwa Brasil kufungwa 7-1 na Ujerumani bali ni mfululizo wa matukio ya ukosefu wa mipango endelevu katika mchezo wa soka.

Tatizo letu sio kocha, tatizo letu sio uwanja bora wa mazoezi, tatizo letu sio jezi nzuri, tatizo letu sio maandalizi mabaya wala matayarisho mabaya.

Yale matatizo madogomadogo ambayo walikumbana nayo wakina Edbily Lunyamila na Mohamed Mwameja leo hayapo tena.

Tumefanikiwa kuyatibu kwa asilimia mia moja lakini wakati tukiangaika kutibu haya magonjwa kuna gonjwa kubwa ambalo limeibuka na hili ndilo haswa linaimaliza Taifa stars.

Tuna gonjwa la kwanza la kutokuwa na wachezaji wanaocheza ligi ya ushindani, kitu kinachopelekea wachezaji kupoteza umakini sana na kwa kiwango kikubwa wakiigharimu timu yetu ya taifa.

Binafsi naamini kwa sasa hatuwezi kulitatua tatizo hili kwa haraka lakini tunapaswa kuwa na wachezaji wazoefu na wa kulipwa angalau kila idara kuanzia eneo la nyuma, kati na eneo la ushambuliaji.

Wakati naendelea kutafakari mara kidogo naiona picha ya Kiraka mpya wa timu ya Azam Shomary Kapombe akiwa analia kwa uchungu.

Nasikitika sana na hapo hapo naanza kucheka kwa hisia za mbali sana. Mara nyingi Chozi la kushindwa hutoka kwa mtu mwenye kiu ya mafanikio lakini akayakosa kwa bahati mbaya. Sasa nikajiuliza huyu Kapombe je kweli ana kiu ya mafanikio?

Wakati akijua kabisa Tanzania tunakosa wachezaji makini wa kulipwa yeye alipata nafasi ya kucheza soka la kulipwa ufaransa lakini akakubali kurudi nyumbani kwa sababu ambazo hadi leo kwa kijana mdogo kama yeye ambaye ni mpambanaji sio za msingi kabisa.

 Unajua kwanini siku hizi Taifa Stars hatuna shida ya kufunga magoli? ni simple tu kwa maana jibu kila mtu analijua ni uwepo wa wachezaji mahiri wanaopiga mpira TP mazembe Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.

Ili tufanikiwe kusonga mbele tunahitaji angalau wachezaji wawili wa kulipwa katika kila idara. Hili litatusaidia kupunguza tatizo la kufungwa magoli ya kizembe kila tunapocheza. Mbali na yote bado tuna nafasi ya kusonga mbele zaidi kama TFF watakuwa na mipango endelevu katika hili.

Makala yangu ijayo ntaelezea njia za kulitatua hili tatizo. MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI TAIFA STARS

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!